Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson
Akizungumza jana Bungeni Mjini Dodoma, Dkt Tulia amesema kanuni zinataka kiti cha spika kutumia madaraka yake kuhakikisha kanuni hazikiukwi na kama amekosea na kwa kuwa yeye ni mwanadamu kanuni zinatoa fursa ya kukata rufaa.
Naibu Spika amesema kuwa kanuni hizo zinataka mlalamikaji kupeleka madai yake kwa katibu wa Bunge ambaye atawasilisha kwa kamati ya Kanuni na kama yanamhusu spika,Kiongozi huyo wa Bunge atatakiwa kuacha kuongoza kikao cha kamati hiyo.
Baada ya Spika kuondoka katika nafasi ya kuongoza Kamati hiyo wajumbe wa kamati hiyo hutakiwa kumchagua mwenyekiti ambae ataongoza kamati hatua ambayo wabunge wanaomlalamikia hawajaichukua.