Jumatano , 25th Jan , 2023

Mahakama ya  mwanzo Msimbati, wilaya ya Mtwara imekosa wateja kutokana na kuwapo kwa Mzee  Issa Mkumba (60), ambaye pia ni Mwenyekiti wa kitongoji cha Mtandi Majengo, ambaye anaaminiwa na jamii yake kutokana na uwezo wake mkubwa wa  kutatua migogoro licha ya kutokuwa na taaluma ya sheria

Ikiwa hii ni wiki ya sheria yenye kauli mbio inayosema,   umuhimu wa  utatuzi wa migogoro kwa njia ya usulushi wajibu wa mahakama na wadau,   kwa Mkoa Mtwara uzindua  umefanyika katika  Mahakama kuu kanda ya Mtwara, ambapo  inabainika kuwapo kwa kesi chache katika mahakama ya Mwanzo Msimbati, baada ya kugundua  uwapo kwa Mzee Issa Mkumba,   ambaye amekuwa akitatua migogoro kwa wakazi wa eneo hilo, 

 Jaji  Mfawidhi  Mahakama kuu Kanda ya Mtwara Zainabu Muruke, ametoa rai kwa wakazi wa Mkoa wa Mtwara, kutatua migogoro yao kwa njia ya usuluhishi, badala ya kukimbilia mahakamani ambapo wamekuwa wakipoteza muda mwingi, na kushindwa kufanya kazi  za kujiingizia kipato.