Jumanne , 12th Jan , 2016

Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, unatariwa kuwasili nchini mwishoni mwa wiki hii.

Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kisha kurejea CCM ,Leticia Nyerere aliyefariki dunia katika hospitali ya Doctors Community iliyopo Lanham, Maryland nchini Marekani unatariwa kuwasili nchini mwishoni mwa wiki hii.

Akizungumza leo nyumbani kwa Mama Maria Nyerere jijini Dar es salaam, msemaji wa familia Joseph Butiku amesema taratibu za kuanza kuusafirisha mwili wa marehemu zinaendelea huko nchini Marekani.

Butiku ameongeza kusema kuwa mara mwili huo utakapowasili nchini kutafanyika ibada ya ya mazishi na kutoa fursa ya watanzania kutoa heshima za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda Butiama kwa mazishi.