Alhamisi , 24th Dec , 2015

Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage amewataka wasimamizi na watafiti wa wizara yake kuhakikisha Tanzania haiingizi bidhaa zisizokidhi viwango ili kuhakikisha Tanzania inasonga mbele kiuchumi.

Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage

Mh. Mwijage ameyasema hayo Jana Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake katika shirika la utafiti na maendeleo ya viwanda (TIRDO), pamoja na shirika la viwango nchini TBS.

Pia waziri Mwijage ametoa agizo kwa TBS na TIRDO, la kutaka udhibiti wa bidhaa feki pamoja na kushirikiana katika tafiti zinazohusu bidhaa zote zinazotumiwa na watanzania.

Naye mkurugenzi wa TBS amesema kuwa changamoto kubwa wanayokumbana nayo katika kuhakikisha kazi zao zinaenda kwa ufanisi mkubwa ni kuwa na bajeti ndogo ya kuwawezesha hivyo kumuomba waziri huyo kuwasadia katika suala hilo.