Jumanne , 5th Apr , 2022

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea kujenga barabara na kutekeleza miradi mingine pamoja na kulipa madeni ya miradi ya nyuma na inayokamilika.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba na Mbunge Halima Mdee.

Mwigulu ameyasema hayo leo Machi 5, 2022 bungeni Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza kutoka kwa mbunge Halima Mdee.
 
Swali la Halima Mdee lilihoji, ''Katika mwaka wa fedha serikali ilitenga Trillioni 1.5 kwenye wizara ya ujenzi, mpaka march mmepewa 68% ambayo ni Trillioni 1.09, hakuna barabara mpya hata moja iliyojengwa katika kipindi hiki, kwanini msieleze mwaka huu tunalipa madeni na mwakani tunajenga barabara kuliko kuwapa majibu mazuri mazuri''.

Majibu ya Mwigulu Nchemba yalikuwa hivi, 'Kinachofanyika tunatekeleza mradi kazi inapokamilika mkandarasi analipwa, na tunaendelea na miradi mipya na yenyewe kadri certificate zinapokuja tunalipa. Inawezekana madeni yakawepo lakini tunafanya uhakiki tunalipa''.

Áidha akaongeza kwa kusema, ''Inawezekanaje tujenge reli inayokwenda mpaka bara jingine na upande mwingine wa bahari halafu tukashindwa kujenga barabara? hatuwezi kuacha kutengeneza barabara au miradi mipya, tutalipa madeni na tutatekeleza miradi mipya''.

Tazama Video hapo chini