Jumatano , 28th Apr , 2021

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa na Katibu Mkuu wake, Dkt. Hassan Abbasi wamekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mwigulu Nchemba kuhusu namna ambavyo Michezo ya Bahati Nasibu (Sport Betting Nationary Lottary).

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa (kushoto) na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mwigulu Nchemba (kulia)

Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Kambarage, Hazina jijini Dodoma, kilikuwa juu ya michezo hiyo inavyoweza kuchangia maendeleo ya michezo na uchumi wa nchi kwa ujumla.

Hatua hii ni mkakati mahususi wa kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan la kutaka kuzalisha ajira kwa vijana kupitia Michezo na Sanaa.

Viongozi Wakuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Wizara ya Fedha na Mipango.

Rais Samia katika Hotuba yake bungeni wiki iliyopita aliweka wazi kuwa Michezo na Sanaa ni miongoni mwa sekta zinazo toa ajira kwa vijana wengi Tanzania.