Jumapili , 2nd Jan , 2022

Mwanasheria Mkuu wa kwanza wa Kenya aliyekaa ofisini kuanzia 1963 hadi 1979, Charles Mugane Njonjo, amefariki Dunia leo Jumapili Januari 2, 2022 akiwa na miaka 101.

Hayati Charles Mugane Njonjo

Familia yake imesema amefariki akiwa nyumbani kwake Muthaiga Nairobi, baada ya kusumbuliwa na Nimonia.

"Ni kwa masikitiko makubwa kwamba asubuhi ya leo, Jumapili tarehe 2 Januari 2022, nimepokea taarifa za kuhuzunisha za kufariki kwa Charles Mugane Njonjo," - Rais Uhuru Kenyatta akitangaza kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe Charles Mugane Njonjo.

Charles Mugane Njonjo alistaafu kama mwanasheria mkuu akiwa na umri wa miaka 60.

Baadaye Njonjo alichaguliwa bila kupingwa katika Bunge la Kitaifa Aprili 1980 kama Mbunge wa Jimbo la Kikuyu.

Aliyekuwa rais Hayati Daniel Moi alimteua katika Baraza la Mawaziri mnamo Juni 1980 kuhudumu kama Waziri wa Masuala ya Ndani na Kikatiba.