Alhamisi , 25th Oct , 2018

Bi. Sahle-Work Zewde ameweka historia nchini Ethiopia baada ya kuteuliwa kuwa Rais wa nne na wa kwanza mwanamke nchini humo, muda mfupi baada ya Rais wa nchi hiyo Mulatu Teshome kujiuzulu wadhifa wake.

Kabla ya kuteuliwa kwake Bi. Zewde alikuwa Balozi na mwanadiplomasia wa kimataifa ambaye aliitumikia Ethiopia na taasisi mbalimbali za kimataifa.

Tukio hili limetokea siku chache baada ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo Abiy Ahmed kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri na kuteua wanawake wengi zaidi, jambo ambalo halijawahi kutokea kwenye historia ya nchi hiyo inayokumbwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe mara kwa mara.

Baada ya tukio la kubadilishwa kwa Baraza la Mawaziri, hapo jana aliyekuwa Rais wa nchi hiyo  Mulatu Teshome aliandika barua ya kujiuzulu, na bunge kuipitisha rasmi mapema leo.