Jumatatu , 4th Dec , 2023

Polisi nchini Kenya wamemkamata mwanamke mmoja anayetuhumiwa kumtupa mtoto wake wa miezi minane katika bahari ya Hindi siku ya Jumapili.

Mashuhuda waliambia vyombo vya habari vya eneo hilo kwamba mwanamke huyo anadaiwa kumtupa mtoto huyo baharini kutoka kwenye kivuko alipokuwa akitia nanga katika mji wa pwani wa Mombasa.

Video ya wapiga mbizi wakimwokoa mtoto huyo imesambaa katika mitandao ya kijamii, na kusababisha Wakenya wengi kuonyesha hasira dhidi ya mwanamke huyo na afueni kwa usalama wa mtoto huyo.

"Alikimbizwa kwa huduma ya kwanza katika Kituo cha Msalaba Mwekundu, alitibiwa na kuruhusiwa katika hali nzuri na mama yake alipelekwa kituo cha polisi kwa mahojiano," K24 inayomilikiwa na kibinafsi na Citizen TV zote zimeripoti, wakinukuu ripoti ya polisi ya tukio hilo.

Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya awali lilisema kuwa mtoto huyo yuko salama katika kituo chake cha uokoaji.

Bado haijafahamika ni mashtaka gani, ikiwa yapo, yatawasilishwa dhidi ya mwanamke huyo.