Jumatatu , 20th Mar , 2023

 Mkazi wa Kijiji cha Kiperesa, Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, Sophia Ishuka (56) amejinyonga kwa mtandio akiwa nyumbani kwake kwa madai kuwa mimea yake imeathirika kwa kiwango kikubwa shambani kwake baada ya  mvua kukosekana. 

Imeelezwa baada ya kufika shambani kwake Machi 19.2023 Bi. Sophia alikuta hali mbaya ya mimea hali iliyompelekea kuanguka ghafla na kupoteza fahamu ambapo baaaye alizindukana kurejea nyumbani kwake.

Alipofika nyumbani kwake alieleza majirani zake mkasa na kilichompata akiwa shambani kisha kuingia ndani ya nyumba yake na kujinyonga

Diwani wa Kata ya Kiperesa Habibu Kiberenge ameelezea tukio hilo kuwa ni la kusikitisha akisema tayari ameshajulisha Jeshi la Polisi Kiteto, na kwamba kinachosubiriwa ni  wao kufika kwao hapo Kijijini kwa hatua zaidi.