
Elizabeth Valerio alifanikiwa kupinga uamuzi wa Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe kukataa karatasi zake za uteuzi.
Maafisa walisema kuwa alishindwa kulipa ada ya uteuzi ya dola elfu ishirini sawa na zaidi ya shilingi milioni nane za Kitanzania .Katika kesi yake mahakamani, Bi Valerio alidai kuwa alikuwa ametoa ushahidi wa uhamisho wa benki.
Mapema mwezi huu alisema kuwa wanawake nchini Zimbabwe wananyimwa fursa ya kushiriki.Kwa sasa kuna wagombea 12 wa urais huku uchaguzi huo ukitarajiwa kufanyika Agosti 23.