Jumanne , 12th Feb , 2019

Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro linamshikilia Kereto Likoko kwa madai ya kumuua Mwanafunzi Samson Conradi anayesoma katika Chuo cha Faraja kwa kumkata na sime shingoni kwa madai ya kushindwa kumlipa fedha ya pete ambayo alikuwa akiuza.

Pete.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa taarifa za awali zinaonyesha kuwa kabla ya kifo marehemu akiwa na mwanafunzi mwenzake, Andrew Charles, walikuwa katika mazungumzo ya kuuziwa pete na mtuhumiwa huyo.

Wakati wakiendelea na mazungumzo hawakuelewana na mtuhumiwa akitaka kupatiwa fedha yake, na alichomoa sime na kumjeruhi marehemu shingoni ambapo ilipelekea kuvuja damu nyingi na amefariki dunia,” amesema Kamanda Issah.

Katika hatua nyingine Kamanda Issah amethibitisha pia vifo vya watu watatu katika mazingira tofauti ambapo mmoja wapo amekutwa amejinyonga ndani.

Bofya link hapo chini kumskiliza Kamanda Issah amefunguka zaidi.