Ijumaa , 17th Mar , 2023

Mwalimu Emmanuel Chacha maarufu kama Dizzo, amefariki dunia kwa kuchomwa kisu na mwalimu mwenzie anayefahamika kwa jina la Samweli Subi akiwa katika usimamizi wa mitihani ya KKK ya darasa la kwanza katika shule ya msingi Igaka mkoani Geita,

Inaelezwa kuwa muuaji amekiri kosa na chanzo kikielezwa ni kugombea nafasi ya uongozi
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na mtuhumiwa tayari amekamatwa na kukiri kutekeleza tukio hilo huku chanzo kikihusishwa kugombea nafasi ya uongozi