Ijumaa , 26th Jul , 2024

Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam imetoa hukumu ya kesi iliyokuwa imefunguliwa na Wakili wa kujitegemea Boniface Mwabukusi dhidi ya TLS (Chama cha Mawakili Tanganyika).

Wakili Boniface Mwabukusi, Mgombea urais TLS

Wakili Mwabukusi alikuwa akipinga uamuzi wa kamati ya rufani kumuengua kugombea nafasi ya Rais wa chama hicho katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi Agosti mwaka huu.

Katika hukumu iliyotolewa  leo, Ijumaa Julai 26.2024 na Jaji Butamo Phillip, mahakama imeeleza kuwa imeridhika na hoja zilizotolewa na upande wa Mwabukusi ambapo sasa rasmi imetengua maamuzi ya kamati ya rufani ya TLS, hivyo kwa sasa Wakili Mwabukusi amerejeshwa kugombea nafasi ya Rais wa TLS.

Mwabukusi alikuwa mmoja wa wanachama walioomba na kupitishwa na Kamati ya Uchaguzi kugombea nafasi ya urais wa TLS, lakini akapingwa kwenye kamati ya maadili ambayo ilimwengua.