Jumatatu , 8th Apr , 2024

Jeshi la Polisi nchini limethibitisha kutokea kwa vifo vya watu 15 ambao wamesombwa na maji  kufuatia mvua znazoendelea kunyesha katika maeneo mbambali nchini ambapo kat ya watu hao, 12 ni watoto na watatu ni watu wazima.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David A. Misime - DCP

Taarifa iliyotolewa na Jeshi hilo inaeleza kuwa watu hao, wengine wamefariki wakiwa wanaogelea, wengine wakiwa wanavuka maeneo ambayo maji yanatiririka kwa kasi na wengine kutokana na kutumbukia kwenye mashimo/madimbwi yaliyojaa maji.

Matukio hayo yametokea katika Wilaya  mbalimbali hapa nchini. Wilaya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa mtu mmoja mwanaume miaka 18, alisombwa na maji ya mvua yaliyokuwa yakitokea milimani wakati akijaribu kuvuka daraja Aprili 1,2024.

Tarehe hiyo hiyo katika Wilaya ya Kilwa Mkoa wa Lindi watoto 2 wote wakiwa na miaka 12 walikufa maji baada ya kusombwa na maji ya mvua.

Aprili 2,2024 mwanaume mmoja wa miaka 28, huko katika Wilaya ya Ludewa Mkoa wa Njombe alikufa baada ya kufukiwa na udongo ulioporomoka kutokana na mvua kubwa zilizokuwa zinanyesha.

Aprili 3,2024 huko Wilayani Muheza Mkoa wa Tanga, mtoto wa miaka 8 alikufa maji wakati akiogelea.
Aidha, katika taarifa hiyo inaeeleza kuwa Aprili 5, 2024 mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 55 huko Wilayani Babati moani Manyara alifariki dunia baada ya kutumbukia kwenye shimo lenye maji.

Kufuatia matukio hayo kwa mwezi huu na  katika kipindi kifupi na uzoefu wa matukio mengine kama haya ya siku za nyuma Jeshi la Polisi limetoa wito na tahadhari kwa watu wote hususani wazazi na walezi kuwalinda watoto kwa karibu sana na kuwapa maelekezo sahihi kutokana na mvua hizi zinazoendelea kunyesha.