Alhamisi , 14th Oct , 2021

Mwanaume aitwaye Masten Wanjala, aliyekiri kuwaua zaidi ya watoto 10 nchini Kenya, ametoroka kwenye kituo cha polisi alichokuwa anashikiliwa cha Jijini Nairobi. Jana Jumatano ya Oktoba 13, 2021, Wanjala alitarajiwa kufikishwa mahakamani kufuatia matukio yake ya mauaji.

Masten Wanjala, Muuaji wa watoto zaidi ya 10

Msako mkali umeanza kumtafuta mtuhumiwa huyo baada ya polisi kubaini hayupo rumande wakati walipokuwa wanaitisha majina asubuhi.

Wanjala alikuwa anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi wa mauaji ya mfululizo ya watoto yaliyolishtua taifa la Kenya.

Polisi waliokuwa zamu wakati mtuhumiwa huyo anatoroka kwenye kituo cha Jogoo Road eneo la Eastlands Jijini Nairobi wamekamatwa.