Dkt. Fenella Mukangara Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu nchini Tanzania THRDC umesema kupitishwa kwa muswada wa sheria ya vyombo vya habari ya mwaka 2015 iliyoandikwa bila kufanyiwa marekebisho ni ukiukwaji wa haki za binadamu na kuinyima sauti katika kutetea haki za binadamu.
Akiongea leo jijini Dar es salaam, wakili wa THRDC Boka Lyamuya amesema wao kama watetezi wa haki za binadamu na wanasheria wameanza harakati mbalimbali za kuhakikisha mswada huo unafanyiwa marekebisho makubwa katika vipengele vinavyokiuka haki za binadamu.
Lyamuya amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazo sisitiza uhuru wa Vyombo vya habari,lakini mswada huo unapingana na uhuru huo pamoja na haki za kupata habari kutokana na muswada huo kuvitaka vyombo vyote nchini kuungana na Idhaa ya taifa wakati wa taarifa ya Habari.