Jumapili , 3rd Feb , 2019

Mwanamuziki Bobi Wine ambaye pia ni mbunge nchini Uganda amesema atawania urais nchini humo katika uchaguzi mkuu ujao akidhamiria kumwondosha madarakani, Rais Yoweri Museveni.

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni.

Bobi Wine ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, amekiambia kituo kimoja cha televisheni cha Marekani kuwa amejiandaa kumkabili Rais Museveni.

Alipoulizwa kama ana uwezo wa kukabiliana na Rais aliyekaa madarakani kwa muda mrefu, mwanasiasa huyo anayewavutia vijana wengi alijibu, “Tuna Waganda wengi waliojiandikisha kama wapiga kura wapya, na hii ndiyo njia pekee ya kumwondosha Museveni na watu wengi wamekuwa wakija kwangu wakitaka niwanie nafasi hii".

Bobi Wine

Museveni alishinda katika uchaguzi uliofanyika 2016 na kulingana na matakwa ya katiba hakuruhusiwa kuwania tena madaraka kutokana na umri wake lakini marekebisho yaliyofanyika baadaye yalimwondolea kizingiti hicho.