Jumatatu , 4th Sep , 2023

Juma Peter mkazi wa Nyamhimbi wilayani Bariadi mkoani Simiyu, anatuhumiwa kumuua na kisha kumfukia mke wake ndani ya chumba walichokuwa wanalala na mara baada ya kufanya tukio hilo aliuza eneo hilo ambalo lilikuwa na nyumba ya tope na kuhamia sehemu nyingine.

Mwili ukiwekwa ndani ya gari

Hali hiyo imebainika hii leo baada ya mtu aliyenunua eneo hilo kuanza shughuli za ujenzi ambapo leo wakati wachimbaji wakiendelea na zoezi la kuchimba msingi wakakutana na fuvu la kichwa cha binadamu.

Kwa mujibu wa mafundi hao wamesema wakati wakiendaelea na zoezi la ukamilisha wa uchimbaji wa msingi huo ambao walianza kuuchimba siku ya Jumamosi ndipo walipokutana na fuvu la kichwa cha mtu hatua iliyopelekea kutoa taarifa kwa fundi mkuu na fundi mkuu kumjulisha mtu mwenye kiwanja na mara baada ya mmiliki wa kiwanja kufika waliwaita viongozi wa mtaa ambao walilazimika kuwapigia simu polisi na mtuhumiwa kukamatwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Nyamhimbi amesema mtuhumiwa alikuwa na tabia ya kuoa wanawake na kuacha huku Afisa Afya wa Halmashauri ya mji akithibitisha mwili huo kuwa wa mwanamke, ambao umezikwa kwa zaidi ya mwaka mmoja.