Alhamisi , 7th Jul , 2016

Katika Sherehe ya Iddi el Fitri iliyoasharia kuisha kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani Dunia kote waumini wa Dini ya Kiislam Mkoani Mtwara wamesheherekea sikukuu hiyo kwa kuchangia damu.

Wachangiaji damu (Picha na Maktaba)

Zoezi hilo la kuchangia damu limemalizika mara baada ya kufanyika kwa ibada iliyofanyika katika viwanja vya shule za sekondari ya amana na kuhudhiriwa na idadi kubwa ya waumi wa dini hiyo.

Wakizungumza mara baada ya kufanyika kwa zoezi hilo waumi hao wamesema kuwa kuchangia damu ni sehemu ya ibada kwa kuwa inatumika katika kuwajali watu wenye mahitaji ya muhimu ya damu salama katika kupata matibabu.

Kwa upande wake Afisa Uhamasishaji uchangiaji wa damu Kanda ya Kusini, Mary Meshi amesema kuwa damu hiyo itasaidia kwa kiwango kikubwa kutokana na benki ya damu katika mkoa kupungua kwa kiasi kikubwa.

Katika hatua nyingine baadhi ya waislam walioshiriki katika ibada hiyo wamewataka Watanzania kudumisha amani na Utulivu huku wakiwakata kuendeleza matendo mema waliyokuwa wakiyafanya mwezi wa mtukufu Ramadhani.