Ijumaa , 22nd Mar , 2024

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amemteua mtoto wake Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuwa Mkuu mpya wa Majeshi (CDF) nchini Uganda nafasi ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Jenerali Wilson Mbasu Mbadi ambaye alimteua kuwa Waziri wa masuala ya biashara.

Jenerali Muhoozi Kainerugaba Mkuu mpya wa Majeshi (CDF) wa Uganda

Uteuzi huo umefanyika usiku wa kuamkia Machi 22, 2024 katika mabadiliko ya Baraza ambayo Rais Museveni ameayafanya na kuacha maswali mengi juu ya nafasi ya CDF kuchukuliwa na mtoto wake. 

Awali kabla ya uteuzi huu Jenerali Muhoozi alikuwa akihudumu nafasi ya mshauri mkuu wa Rais katika masuala ya operesheni maalumu.

Itakumbukwa kuwa Jenerali Muhoozi aliwahi kuwa kwenye nafasi ya Ukamanda wa Jeshi la Ardhini la Uganda lakini October 04,2022 Museveni aliamua kumuondoa na nafasi yake ikachukuliwa na Meja Jenerali Kayanja Muhanga ambaye alikuwa Kamanda wa Opereshemi Shujaa inayoendeshwa Nchini DRC.