Jumapili , 14th Nov , 2021

Mtoto wa miaka sita Eric Joshua Mkandi mkazi wa kitongoji cha Mkapa kijiji cha Izumangabo kata ya Bwanga,  mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Izumangabo amefariki kwa kujipiga risasi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amesema mtoto Eric amefariki wakati anapatiwa matibabu katika hospital ya Bwanga baada ya kujipiga risasi kwa silaha aina ya Pistol Beretta inayomilikiwa na baba yake kwenye paji la uso na kutokea kisogoni akiwa ndani ya chumba cha baba yake mzazi aitwaye Joshua Mkandi.

Tazama Video hapo chini