Kisima
Akizungumzia tukio hilo Mama mzazi wa marehemu Neema Charles amesema mtoto wake alipotea majira ya saa kumi na mbili jioni ambapo walianza kufanya jitihada za kumtafuta bila mafanikio kesho yake ndipo walipogundua kuwa mtoto huyo ametumbukia kwenye kisima hicho baada ya watu kuona mikono yake.
"Baada ya kukaa muda hatumuoni mtoto tuliamua kuanza kumtafuta tulimtafuta mpaka saa tano usiku wakati natoka nje asubuhi nikakuta watu wengi wengine wamemshikilia mume wangu nikashangaa nikauliza kuna nini hapa wakaniambia pole sana mtoto wenu amedumbukia kwenye kisima yupo mule," amesema Mama mzazi
"Hiki kisima sio mara ya kwanza kinapoteza watoto yaani hapa kilipo hata mtu mzima kama amelewa umekunywa pombe unaweza kuangukiamo ila polisi amekuja hapa ameagiza wenye visima lazima waviweke kwenye mazingira mazuri sio mazingira ya kutatanisha kama haya," wamesema
Wakazi wa Mtaa wa Nyampa wanaiomba serikali kuwawajibisha wamiliki wa nyumba ambao wanaacha mashimo ya vyoo na visima wazi jambo ambalo linahatarisha maisha ya watoto wao.