Ijumaa , 11th Jun , 2021

Binti mdogo kuliko wote Afrika kupanda Mlima Everest, ambaye pia ni Mtanzania Rawan Dakik, amesema zoezi alilofanya la kupanda Mlima KIlimanjaro kwa zaidi ya mara tano limechangia kufanikiwa kwake kupanda mlima huo mrefu zaidi duniani wenye urefu wa mita 8,850 kutoka usawa wa Bahari.

Mtanzania Rawan Dakik akikabidhiwa Ua na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Mary Masanja

Rawan ameyasema hayo leo asubuhi mara baada ya kuwasili nchini akitokea nchini Nepal kwenye zoezi hilo lilochukua miezi miwili, ambapo amepokelewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Mary Masanja, ambapo ameeleza kufurahishwa na hatua ya mafanikio ya Rawan na kuwa itakuwa njia nzuri zaidi ya kuutangaza Mlima Kilimanjaro kiutalii kama sehemu bora kwa mazoezi kwa wanaopenda kupanda milima mirefu zaidi duniani.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John Mongela, amepongeza uamuzi huo wa kishujaa wa Rawan kuwa utahamasisha Watanzania wengi zaidi kupenda utalii wa kupanda milima hususan Mlima Kilimanjaro.

Mtanzania Rawan Dakik, alifanikiwa kufika kilele cha Mlima Everest, Mei 23, 2021.