Jumapili , 16th Mei , 2021

Kufuatia uwepo wa changamoto kadhaa katika sekta ya elimu nchini mtandao wa elimu Tanzania (TENMET) umeandaa mkutano wa kimataifa kuzijadili changamoto hizo ikiwemo uwajibikaji wa pamoja katika kugharamia elimu bora.

Wanafunzi

ukihusisha taasisi zote za elimu za juu, taasisi za utafiti wakiwemo mabalozi wanaowakilisha nchi mbali mbali duniani. Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete.

“Kila mwaka tumekuwa tunaandaa mktano wa kujadii ubora wa elimu ambao hutoa fursa kwa wadau wa elimu ikiwemo serikali wananchama wa mtandao wadau wa maendeleo kuona ni namna gani elimu wanayoipata watoto wetu inakwenda kujibu changamoto katika dunia ya leo”amesema Ochola. 

Akizungumza na EATV mapema hii leo mratibu wa mtandao huo wa elimu wamesisitiza kuwa kwa takribani miaka 60 ya uhuru wa Tanzania katika mkutano huo itajadiliwa ni elimu ya aina gani ambayo watanzania wanapashwa kuipata kwa sasa itakayokidhi mahitaji ya sasa ikiendana sambamba na mabadiliko ya Tehama.

Mkutano huu wa kimataifa unatarajiwa kufanyika kwa siku tatu mfululizo kuanzia mei 18hadi 20, 2021 ukihudhuriwa na wadau mbali kutoka ndani na nje ya Tanzania.