Jumanne , 11th Jan , 2022

Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini Dkt. Joseph Kasheku Msukuma amejitosa kuwania nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya leo Januari 11, 2022, kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama Chake cha CCM.

Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini Dkt. Joseph Kasheku Msukuma

Mchakato wa kumpata mgombea ndani ya CCM.

Mchakato wa kumpata spika mpya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Kuanzia tarehe 10-15, linafanyika zoezi la kuchukua na kurejesha fomu kwa wabunge wa CCM kuomba kuteuliwa na chama kuwania kiti cha Spika''.

''Tarehe 17, 2022 sekretarieti ya Halmshauri Kuu ya Taifa itakutana kwaajili ya kujadili wagombea na kuishauri Kamati Kuu juu ya wagombea ambao wamejitokeza kuomba kiti cha uspika''.

''Tarehe 18-19 kutakuwa na kazi ya kuchuja na kufanya uteuzi wa mwisho ambapo kamati kuu ya Halmashauri kuu itafanya kazi hiyo''.

''Kuanzia tarehe 21-30, katika siku hizo, Cocas ya Chama ya wabunge wa CCM itapiga kura kumpata mbunge ambaye atakwenda kusimama bungeni kwaajili ya kuomba kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania''.