Jumatano , 31st Mei , 2023

Serikali imekanusha taarifa za upotoshaji zilizotolewa na mtandao wa myflylight.com kuhusu ndege ya mizigo ya ATCL aina ya Boing 767-300F kukamatwa ikiwa na inasafirisha shehena ya mizigo haramu ambayo haijafuata taratibu za kiforodha.

Ndege

Ufafanuzi huo umetolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, ambapo amesema taarifa iliyotolewa na mtandao huo ilieleza kuwa sekta ya anga Tanzania imekumbwa na kashfa nzito ya ndege yake na kwamba taarifa hiyo ina lengo la kurudisha nyuma juhudi za serikali.

"Nataka niwaambie kwamba taarifa hizo ni za upotoshaji na uzushi mkubwa na zipuuzwe, serikali inaona kama taarifa hizi ni njia mojawapo ya kurudisha nyuma juhudi zake za kukuza sekta ya usafiri wa anga ni za upotoshaji kwa sababu hazina ukweli wowote," amesisitiza Msigwa.

Aidha Msigwa amesema ndege hiyo bado haijafika Tanzania na haijaanza rasmi kazi zake