Jumapili , 8th Mar , 2020

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, amesema kuazia leo Machi 8, 2020, ataanza kuwashughulikia wanaume wenye tabia ya kuwapiga wanawake hadi kuwaharibu mwonekano wa sura na baadhi yao kuwasababishia ulemavu wa kudumu.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Makonda amesema mwanamke yeyote atakayeshushiwa kipigo na mwanaume, kuanzia sasa atoe taarifa kupitia simu ya mkononi namba 0682009009 ili mwanaume alietenda ukatili huo, atafutwe popote alipo na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Aidha Makonda amepanga kuliomba Bunge la Tanzania, linapofanya mabadiliko ya sheria ya ndoa, kiongezwe kipengele cha kukata asilimia 40 ya mshahara wa mwanaume, apatiwe mwanamke ambaye anajishughulisha na kazi za nyumbani, ili ikifika mwishoni mwa mwaka kila mmoja awe na cha kwake.