Jumatano , 11th Mar , 2020

Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, amewaomba wananchi kuendelea kutoa michango yao ili kuwanusuru viongozi wa chama hicho waliohukumiwa siku ya jana kulipa faini ama kifungo cha miezi mitano jela na kwamba baadaye chama hicho kitafanya kikao ili kujua kiasi kilichopatikana.

Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema

Akizungumza leo Machi 11, 2020 na EATV&EA Radio Digital, Mbunge Lema amesema kuwa anawashukuru wananchi wote waliojitoa hadi hapo zoezi hilo lilipofikia.

"Hakuna sekunde hata moja ambayo siwezi kupokea simu kwa watu wanaotaka kuchangia, tuseme tu jambo hili litafanikiwa kwa asilimia 100 watu waendelee tu kuchanga fedha kwa wingi na tuoneshe kwamba msamiati wa kushindwa kwetu hakuna" amesma Lema.

Viongozi nane wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wao Freeman Mbowe, jana walihukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam, kulipa faini ambayo ni zaidi ya Shilingi Milioni 300, ama kifungo cha miezi mitano jela.