Alhamisi , 22nd Sep , 2022

Baada ya Serikali kushirikiana na shirika la umoja wa Mataifa la chakula Duniani FAO na Umoja wa Ulaya EU kuzindua mradi wa kuimarisha huduma za afya ya mimea na usalama wa chakula wananchi wamehakikishiwa mazao yanayotoka na kuingia nchini yanakuwa na ubora

Naibu Waziri wa Kilimo  Anthony Mavunde akizindua mradi huo amesema utasaidia katika kudhibiti visumbufu vigeni kwa kuhakikisha mazao yanayoingia au kutoka nchini yanakuwa na ubora unaokidhi viwango vya kimataifa

Awali Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu nchini TPHPA Dkt. Efraim Njau amesema sekta ya kilimo imeajiri zaidi ya asilimia 67 ya Watanzania na kuchangia takribani asilimia 29 ya pato la taifa huku mwakilishi  mkazi wa FAO Nyebenyi Tipo amesema mradi huo unalenga kuhakikisha usalama wa chakula hasa mazao