Jumapili , 18th Feb , 2018

Mgombea Ubunge wa jimbo la Siha kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk. Godwin Mollel ameibuka mshindi wa kiti hicho baada ya matokeo yaliyotangazwa usiku w kuamkia leo.

Katika uchaguzi huo mdogo ambaop umefanyika jana katika majimbo mawili ikiwemo jimbo la Kinondoni Mollel amepata kura 25,611 na akimshinda mpinzani wake mkuu  Elvis Mosi wa CHADEMA aliyepata kura 5,905.

Tayari Tume ya Uchaguzi (NEC), imetamtangaza rasmi Dk Godwin Mollel kuwa mshindi wa uchaguzi huo mdogo wa Ubunge, Jimbo la Siha mooani Kilimanjaro na atakuwa mwakilishi wa wananchi wa Siha bungeni hadi mwaka 2020.

Kabla ya kugombea kupitia Chama Cha Mapinduzi Dr. Mollel ndiye alikuwa Mbunge wa Jimbo hilo kuanzia mwaka 2015 kupitia CHADEMA ambapo alitangaza kuhama chama hicho mwaka jana na kujiunga na CCM pamoja na kujiuzulu Ubunge.