Jumatatu , 2nd Jun , 2014

Mbunge wa Ubungo, Mhe. John Mnyika leo ametaka kuahirishwa kwa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maji mpaka hapo fedha zitakapoongezwa kwenye bajeti ya wizara hiyo, fedha alizodai kuwa zimekuwa ni ahadi hewa.

Mbunge wa Ubungo John Mnyika.

Akichangia katika kikao cha Bunge, mjini Dodoma kuhusu makadirio ya Bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2014/2015 amesema anakusudia kuweka mezani hoja hiyo juu ya kauli iliyotolewa na waziri wa maji ilikutathmini ukweli wa utekelezwaji wa miradi ya maji.

Mhe. Mnyika amesema mradi katika mtambo wa Ruvu Juu umeathiri kwa kiasi kikubwa wakazi wa jiji la Dar-es-Salaam kutokana na maji yanayofika jijini kutokidhi uhitaji wa wakazi wa jiji.