Alhamisi , 13th Mei , 2021

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Christine Mndeme, amesema kuwa yeye alijengewa ujasiri tangu akiwa mdogo na kwamba hiyo ilimsaidia hata kuweza kutatua mgogoro wa wafugaji na wakulima ambao walikuwa na silaha kali na aliweza kuingia katikati ya wanaume hao na kuzungumza nao.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Christine Mndeme

Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 13, 2021, kwenye kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Radio na kusisitiza kuwa wanawake wanapaswa kujiamini kwani kila analoliweza mwanaume na mwanamke analiweza.

"Nilipokuwa Mkuu wa wilaya fulani kulitokea mapigano makubwa ya wakulima na wafugaji nilienda mwanamke mwenyewe katikati ya wanaume wakiwa na silaha kali za kijadi na nilitatua ule mgogoro na niliwauliza mbona mko wanaume tu, wakanijibu wanawake wapo nyumbani sisi ndiyo tunapambana," amesema Mndeme.