Jumatatu , 24th Mar , 2014

Wakazi wa mji wa Moshi Mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania wamepatwa na adha kubwa ya usafiri kuanzia asubuhi ya leo kufuatia mgomo wa madereva wa daladala na mabasi yaendayo Arusha kupinga faini kubwa zinazotozwa na trafiki.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama amelazimika kuingilia kati suala hilo na kufanya mkutano na wadau katika kuhakikisha kuwa hali ya usafiri inarejea kawaida.

Aidha mkuu huyo wa mkoa amezungumzia pia adha zilizowapata wananchi wananchi wa Moshi na Arusha na hatua ambazo uongozi wa mkoa umechukua ili kumaliza mgomo huo: