Jumatano , 5th Aug , 2015

Ilikuwa leo Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim azungumze na Wanahabari asubuhi hii ila mkutano huo umehairishwa hadi siku nyingine tena.

Magdalena Sakaya ameulizwa Prof. Lipumba alitaka kuzungumza nini na akajibu wao hawajui kitu alichotaka kuwaambia wananchi

Sababu kubwa ya kusitishwa mkutano, Magdalena amesema Wazee wa CUF wametaka kujua kwanza ni kitu gani Mwenyekiti anataka kuongea

Wananchi nje ya ofisi za CUF wanashangilia wakiimba kwa kusema 'Si mnaona, muziki wa Lipumba kuuzima hamuwezi'

Mmoja wa Wananchi wanaoshangilia amesema wamefurahia kwakuwa wanaamini Mwenyekiti wao Lipumba hajiuzulu na yuko na wananchi.

Wananchi tofauti wanaoshangilia wanasema wanamuamini Lipumba na dalili iliyopo ni kuwa hawezi jiuzulu maana anawasikiliza na ataendelea kuwa Mwenyekiti daima