Jumamosi , 17th Aug , 2019

Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya SADCDr. Stergomena Lawrence ameipongeza Tanzania kuwa nchi pekee ambayo imeongoza kwa kukidhi vigezo vya ukuaji wa uchumi, kwa kufikia asilimia 7, ikiwa ni tofauti na nchi nyingine.

Kauli hiyo ametoa wakati wa mkutano wa kwanza wa SADC uliofanyika jijini Dar es salaam, ambapo viongozi mbalimbali wa jumuiya hiyo wakiwemo viongozi wastaafu na Mawaziri wamehudhuria.

Dkt Lawrence amesema kuwa "uhimilivu wa uchumi ni nyenzo muhimu katika maendeleo, nchi wanachama zimekizi vigezo vya SADC kiuchumi, takwimu zimeonesha TZ inafanya vizuri, na kwa vigezo pekee TZ ndiyo nchi pekee ambayo imefikia ukuaji wa asilimia 7, mjipongeze."

Aidha  Dr. Stergomena Lawrence amesema "katika kufikia uchumi wa Viwanda nchi wanachama hawana budi kukuza uzalishaji wa umeme, kwa kuwa ni kitu muhimu kwenye ujenzi wa viwanda, nashukuru katika wiki ya Viwanda, kuna tumeziona kupitia Mradi wa Umeme wa Nyerere."

Mkutano huo unafanyika kwa siku 2 kuanzia leo Agosti 17 pamoja na Agosti 18.