Jumanne , 5th Feb , 2019

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi mkoani Singida, Pius Luhende na Askari wawili wanashikiliwa kwa tuhuma za kumuua mwanaume aliyejulikana kwa jina la Peter Chambalo kwa kumpiga risasi akiwa kanisani.

Jeshi la Polisi limesema kuliibuka mgogoro, na Askari akafyatua risasi na kumjeruhi Chambalo, ambaye alifariki dunia papo hapo.

Inadaiwa kuwa Mkurugenzi huyo alifika kwenye Kanisa la Waadventista Wasabato akiwa na askari kisha kumshambulia muumini huyo.

RPC alipofika katika eno hilo, ameshangazwa na kitendo cha Mkurugenzi huyo ambapo amehoji ni kwanini afanye kitendo hicho kwenye nyumba ya ibada na katika kipindi kama hiki lakini pia amebainisha kuwa atahakikisha anamfikisha kwenye vyombo vya sheria kwa kuwa hakuna aliyeko juu ya sheria.

Hata hivyo baada ya taarifa hiyo, Mwanaharakati na Rais wa Wanasheria Tanganyika Fatma Karume amekumbusha historia ya nyumba huku akisubiri kuona maamuzi ya DPP.

"Nimesikia DED wa Manyoni/Itigi kampiga risasi raia. Sasa tukumbushane historia kidogo. Ditto Pile alimpiga risasi dereva wa dalaladala na DPP akasema kauli ya  bila ya kukusudia akamtoa rumande. Ili bidi mola aingilie kati. Said Mwamwindj alivyompiga risasi RC alinyongwa, watu na viatu", amesema Fatma Karume.