Kushoto ni Mbunge mteule wa jimbo la Ubungo Kitila Mkumbo na kulia ni aliyewahi kuwa Meya wa Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA Boniface Jacob
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa hati ya ushindi Prof. Kitila Mkumbo, amewashukuru wananchi wa Ubungo kwa kumuamini na kuahidi kwenda kusimamia kero zote zinazowakabili wakazi wa jimbo hilo.
Na huko Iringa Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo la Mufindi kusini mkoani Iringa John Quiman amemtangaza David Kihenzile kutoka CCM kuwa mshindi kwenye nafasi ya ubunge kwa kupata kura 59,793 sawa na asilimia 97.21