
Kijijini Kinamweli
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu ACP Edith Swebe, amesema tukio hilo limetolea Agosti 11,2023 majira ya saa 1:00 asubuhi na kwamba mke wa marehemu bado hajulikani alipo.
"Katika tukio hili watoto wawili wamekutwa wamening'inizwa kwenye chumba wanacholala na wazazi wao, ambapo baada ya uchunguzi dalili zote zinaonesha wamekufa kwa kunyongwa, pia mwili wa baba yao mzazi ulikutwa ukiwa umening'inia juu ya mti kwa kujinyonga, tunaendelea na uchunguzi wa tukio ili kuweza kubaini chanzo cha matukio haya lakini tunaendelea kumtafuta mke wa marehemu ambaye mpaka sasa hajulikani alipo," amesema ACP Swebe
Kamanda Swebe ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa fiche ili kubaini chanzo cha tukio hilo.