Jumatano , 13th Aug , 2014

Jeshi la polisi kupitia programu yake ya ulinzi shirikishi jamii kwa sasa wameanzisha mpango mkakati wa kuwasadia vijana kuachana na utumiaji wa madaya ya kulevya.

Mkuu wa Polisi nchini Tanzania IGP Ernest Mangu.

Akizungumza Jijini Arusha msaidizi wa Polisi kitengo cha polisi jamii wilaya ya Arusha Mary Maswa amesema kwa kuwa vijana wengi kwa sasa mkaoni humo wanaathirika na madawa ya kulevya, wameona bora waanzishe mpango huo maalum ili kuokoa taifa la Tanzania ambalo msingi wake ni vijana.

Kwa upande wao vijana waathirika wa madawa wakiongea jana katika siku ya vijana duniani wameiomba serikali na mamlaka nyingine zinazohusika na kuzuia matumizi ya madawa hayo kudhibiti uingizwaji wake hapa nchini kwa kuwa madhara makubwa wanayapata wao.