
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Union for Mult-party Democrass UMD. Mwajuma Mirambo ameahidi kutoa Huduma za Afya Bure Kwa wanawake wanao kwenda kujifungua tofauti na hali ilivyo Sasa kwani wanawake hutozwa hela ya Vifaa na Madawa.
"Ninashangaa Sana wanawake katika kipindi hiki ndio mnaonekana sana wa maana lakini baada ya uchaguzi mtarudi kuendelea na mateso yenu kama kawaida hivyo nichagueni Mimi Mwajuma nije kubadilisha kabisa hali ya utoaji wa Huduma za Afya hapa nchini" Amesema Mwajuma Mirambo
Maneno hayo ameyasema wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Kibaha katika Eneo la Mwendapole Manispaa ya Kibaha Mkoani Pwani.