.jpg?itok=6QqE_jBI×tamp=1473672917)
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na katibu mkuu wizara ya afya, Dr. Mpoki Ulisubisya katika uzinduzi wa ripoti iliyofanywa juu ya mradi wa kuhudumia watu masikini na kuwajengea uwezo wa kujitegemea katika sekta mbalimbali.
Dr. Ulisubisya amesema, ili kuwa na malengo yenye tija ni vyema tadhimi ifanyike juu ya mafanikio ya mradi inayofanywa na sio kutoa takwimu pekee.
Naye Naye mwakilishi mkazi wa Mariestops nchini bwana Anil Tambay amesema ripoti hiyo inaainisha mafanikio ya miradi iliyofanywa na taasisi 10 katika huduma ya afya ya mama na mtoto, upatikanaji wa maji safi na salama.
Miradi mingine nipamoja na utuzwaji wa mazingira, ujenzi wa vyoo, Elimu na ugawaji wa mbegu bora ambapo mikoa ya Lindi, Mtwara, Dodoma, Pwani na Tanga imenufaika na miradi hiyo.
Miradi hiyo inafadhiliwa na watu wa Austaralia kupitia mpango unaojulikana kama Africa Community Engagement Scheme AACES Tanzania ambao unafikia mwishoni mwa mwezi juni mwaka huu.
Katika hatua nyingine mwakilishi mkazi wa Marie Stopes Tanzania ametoa zawadi wa bajaji kwa vijana 5 kwaajili ya kujiendesha kibiashara pamoja na kuwafikisha kazini wahudumu wa afya waishio pembezoni.