Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko
Dk Biteko amesema hayo Februari 08, 2024 Jijini Dodoma baada ya kushuhudia utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa uzalishaji umeme wa megawati 49.5 kwa nguvu ya maji katika mto Malagarasi mkoani Kigoma.
Vyanzo hivyo vipya ni pamoja na mradi wa Malagarasi ambao utekelezaji wake utachukua miezi 42 na utekelezaji wa mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) ambao kwa sasa umekamilika kwa asilimia 96 na unatarajia kuingiza umeme kwenye gridi ya Taifa mwezi huu.