Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Miradi mikubwa 9 ya kimkakati kutekelezwa Songwe

Ijumaa , 22nd Mar , 2024

Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imekusudia kutekeleza miradi mikubwa 9 ya kimkakati ikiwemo upanuzi wa barabara kuu ya TANZAM kipande cha Igawa – Tunduma (km 218) na Ujenzi wa kituo cha ukaguzi wa pamoja wa magari katika barabara hiyo eneo la Iboya Songwe.

Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Songwe Suleiman Bishanga amesema hayo tarehe 19 Machi 2024; alipozungumza na Kipindi cha TANROADS Mkoa kwa Mkoa kuhusu mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita katika sekta ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja.

Amemtaja mkandarasi anayejenga barabara hiyo ya njia nne kwa utaratibu wa EPC + F ni M/s China Civil and Engineering Construction Coopration (CCECC) kutoka China; ambaye tayari ameshaanza maandalizi ya kuainisha maeneo ya kujenga kambi.

Amesema pia mradi huo utakuwa na barabara za mchepuo (Bypass) ili kuondoa msongamano wa magari hasa malori katikati ya mji.

Amesema miradi mingine ambayo ipo kwenye mipango ya Serikali katika ujenzi ni Barabara ya Mlowo – Kamsamba na Spur Road ya Chitete Makao Makuu ya Wilaya ya Momba (Km 147) na tayari imeshakamilisha ujenzi wa daraja la Momba linalounganisha Mkoa wa Songwe na Rukwa. 

Pia Barabara ya Isongole II – Ngana / Mbeya – Kasumulu hadi Katumbosongwe Km 124). Sehemu ya Kwanza ya Isongole II – Ibungu – Isoko (Km 52.419) ujenzi unatarajia kuanza hivi karibuni kwani zabuni ilishatangazwa na kumpata mkandarasi wa kujenga kwa kiwango cha lami barabara hiyo na ulipaji wa fidia wa mali, nyumba na mazao umeshakamilika ambapo waathiriwa wa mradi wapatao 312 wamelipwa fidia ya jumla ya TZS Milioni 850.269.

Barabara ya Ruanda – Nyimbili – Izilya – Itumba (Km 79) na Mahenje – Haasamba – Vwawa Km 32. Sehemu ya kwanza km 1.2 Mkandarasi aitwae GNMS Contractors C. Ltd kutoka Iringa anaendelea na kazi; sehemu iliyobaki ya Ruanda – Idiwili km 20 imetengwa sehemu nne za km 5 kila moja ambapo ujenzi wa kiwango cha lami wa sehemu hiyo utafanywa na Wakandarasi Wanawake.

Bishanga ametaja mradi mwingine ni Barabara ya Mbalizi – Chang’ombe – Mkwajuni – Saza – Patamela hadi Makongorosi Km 110, Sehemu ya Chang’ombe – Mkwajuni – Saza – Patamela hadi Makongorosi Km 61, Barabara ya Ibungu – Kafwafwa na Itumba – Shigamba – Ibaba – Katengere pamoja na Ujenzi wa madaraja mawili ya Magamba na Namkukwe katika barabara ya Galula – Namkukwe (Km44.3).

HABARI ZAIDI

Bujukano Mahungu John, Mwenyekiti wa Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Tanzania

Waganga wa jadi waungana kukemea ukatili, Geita

Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Mvua zilizoambatana na upepo zimeua watu watano TZ

Muonekano wa Eneo la Somanga baada ya Mawasiliano kati ya Lindi na Dar es Salaam kurejeshwa.

Mawasiliano yarejeshwa barabara ya Dar - Lindi

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga

Kituo cha kupoza umeme kujengwa Tunduma

Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa Songwe Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Charles Bukombe, akizungumza na abiria

"Fungeni mikanda muda wapo safarini" - SSP