Alhamisi , 3rd Mar , 2016

Baadhi ya tamaduni na Mila za Afrika bado zinaonesha kuwa mwanamke hana nafasi ya kuonekana katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo tofauti na kuonekana mama na mlezi wa familia.

Afisa program dawati la Jinsia na watoto kutoka Kituo cha haki za binadamu nchini (LHRC), Bi.Naemy Silayo

Akiongea leo jijini Dar es Salaam, afisa program dawati la jinsia na watoto kutoka kituo cha haki za binadamu nchini (LHRC), Bi. Naemy Silayo katika mahojiano maalum na East Africa Radio amesema kutokana na changamoto hizo jitihada mbalimbali zimeanza kufanyika katika harakati za kumuinua mwanamke nchini.

Amesema kumekuwa na mabadiliko mengi kisheria ya kumlinda mwanamke vilevile kumekuwa na mwanamke kwa wanawake wenyewe kujitokeza na kuwa na utayari wa kufichua vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa na kituo hicho kinatoa elimu ya kupinga ukatili kuanzia majumbani na kulifikia taifa kwa ujumla.

Aidha afisa huyo ameitaka serikali itekeleze sera zake kivitendo ikiwa ni pamoja na kuweka sheria ya elimu ambayo itawafanya watoto wa kike wapewe fursa sawa kielimu.na kuhakikisha inawachukulia hatua kali wale wote wanaofanya vitendo vya ukatili.