Jumatatu , 17th Nov , 2014

Migogoro ya ardhi kati ya wananchi na wawekezaji imendelea kuwa tatizo kubwa Kisiwani Zanzibar baada ya wananchi katika mmoja la eneo alopewa mwekezaji kukataa kuacha kulitumia kwa shughuli zao za uvuvi.

Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Shaarif Hamad

Mgogoro huo umeikumba eneo la mkoa wa kaskazini Unguja ambapo wakaazi wa eneo la kiombamvua wako katika mgogoro wa eneo lao na mwekezaji aliyepewa eneo hilo kwa taratibu zote za serikali ambaye anataka kujenga uwanja wa michezo.

Hali hiyo imesababisha Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Shaarif Hamad kufika eneo hilo na kusikiliza kilio cha wananchi ambapo amesema iko haja ya pande zote tatu zikakaa pamoja na kukubaliana na kupata ufumbuzi ..

Awali mkuu wa wilaya ya Kaskazini B, Khamis Jabir Makame, amesema mgogoro huo ni wa muda mrefu na ulifika hadi ndani ya baraza la wawakilishi na wananchi wakakubali maagizo ya Baraza na kupatikana ufumbuzi ukiwa ni pamonja namwekzaji kutoa fedha milioni 27,kujenga barabara mpya na eneo jipya la uvuvi ambayo yote yamekamilka lakini ilipofika uwekaji saini wananchi wamekataa makubaliano hayo.