
Sheria hiyo inayojulikana kama 'Movable Property Security Act 2017' inatoa fursa kwa kuanzishwa kwa usajili wa mali hizo ambazo benki zinaweza kutumia kuthibitisha umiliki wa dhamana yake.
Rais Kenyatta amesema, Sheria hiyo itakuza uthabiti na uhakika kwa kutoa dhamana ya mali.
Benki zimekuwa zikikataa kutumia mali inayoweza kuhamishwa kama dhamana ya mkopo kutokana na ukosefu wa data ambayo wanaweza kutumia ili kudai mali hiyo.
Sheria hiyo pia itabainisha ni mali gani ambayo inafaa kutumika kama dhamana.