
Baadhi ya mifugo iliyokamatwa
Kamanda Pasua amesema kwamba tukio hilo limetokea Julai 09, 2022, na kusema licha ya mifugo hiyo kukamatwa lakini mmiliki wake hakuonekana mpaka taratibu za kimahakama zilipokamilika na umuazi kutolewa juu ya uharibifu wa mazao hayo ambapo mahakama ya wilaya Siha ilitoa hukumu kuwa mifugo hiyo itaifishwe.
Kamanda Pasua ameitaja mifugo hiyo kuwa ni Ng’ombe 485, Mbuzi na Kondoo jumla yake ni 963 ambapo ameeleza kuwa mifugo hiyo ili haribu ekari hizo za mazao na uchunguzi wa awali umebaini kuwa mifugo hiyo imetoka nje ya mkoa wa Kilimanjaro na kuingia katika wilaya ya Siha bila ya kufuata utaratibu .