Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale, wakati wa uhai wake
Taarifa zimeeleza kuwa Mhandisi Mfugale, alianguka ghafla akiwa kwenye kikao cha kazi ofisi ya Katibu Mkuu Ujenzi Jijini Dodoma, baada ya kudai hajisikii vizuri na akakimbizwa hospitali ya Benjamin Mkapa kwa matibabu lakini mauti yakawa yamemfika.
Pamoja na mambo mengine, Mfugale atakumbukwa kwa uhodari katika ukamilishaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi wa madaraja ya kimkakati ikiwemo daraja la Mkapa, Kikwete, Rusumo, Nyerere, Mfugale na daraja la Kijazi pamoja mengi ambayo yamekalika chini ya usimamizi wake.
