Mohamed Mtoi Kanyawana wakai wa uhai wake
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Lushoto Mkoani Tanga Mohamed Mtoi Kanyawana aliyefariki dunia kwa ajali ya Gari iliyotokea huko Tanga.
Katika Taarifa iliyotolewa na Mtandao wa Chama hicho inasema wanamasikitiko makubwa na chama kinatoa Salamu za Rambirambi kwa Familia na Uongozi wa Juu wa Chadema Makao makuu kwa msiba huo, na ni Kijana ambaye bado walikuwa wanamuhitaji.
Tarifa hiyo inaongeza kuwa walithamini mchango wake wa kujenga Chama Mohamed Mtoi na alikuwa ni tegemeo kwenye nafasi ya Ubunge Jimbo la Lushoto pia kama mratibu wa Kanda ya Kaskazini,
Hivyo wamepata pigo kubwa hasa katika kipindi hiki kigumu kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu. Mungu aiweke roho ya Marehemu Mohamed Mtoi Kanyawana mahali Pema Peponi.

